Tuesday, January 1, 2019
BANA UKE WKO KWA KUTUMIA NJIA HIZI
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike kisha acha kwa usiku mzima mpaka asubuhi. Asubuhi kunywa hayo maji na ule hizo mbegu pia. Fanya zoezi hili mara 3 TU kwa wiki na uenndelee na zoezi hili mpaka kifaa chako kimerudi na kuwa kidogo. Hii inasaidia pia kupunguza uzito. Mhimu – Wanawake wajawazito au wenye saratani ya matiti wasitumie dawa hii.
2. Unga wa mbegu za embe Unga wa mbegu za embe ni dawa nyingine nzuri unaweza kutumia kukaza misuli ya uke wako uliolegea. Ukishakula embe chukua ile kokwa yake ya ndani na uianike juani, ikikauka chukua na uisage upate unga wake. Changanya unga huu na asali kidogo kisha pakaa ndani ya kuta na sehemu yote ya ndani ya uke kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa na uke wako utarudi na kuwa wa kawaida. Mbegu za embe ni chanzo kizuri cha wanga, mafuta, protini, vitamini E, nyuzinyuzi, magnesiamu, vitamini B12, asidi amino nyingi nk.
3. Vitamini E Kwa mjibu wa utafiti kuhusu faida za vitamini E ni moja ya vitamini mhimu sana ambazo ni mhimu kwa ajili ya afya bora ya mwili. Inapendekezwa kama dawa ya kutibu kisukari na shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito. Hata hivyo wanawake wengi hawafahamu ukweli kwamba vitamini E ni dawa nzuri kwa uke mkavu na kufanya kuta za uke zenye afya na nguvu kama itatumika vizuri. Unahitaji upate mafuta ya vitamini E na uwe unaweka ukeni moja kwa moja mara 1 kwa siku mpaka utakapopata uponyaji unaouhitaji. Huwa kama kidonge hivi lakini ni mafuta na kinapasukia chenyewe ndani ya uke na kusambaa bila shida yoyote.
4. Jeli ya mshubiri freshi Kutumia jeli ya mshubiri au aloe vera ni moja ya njia rahisi ya asili ya kukaza uke wako. Kutumia njia hii kwangua jeli (utomvu mweupe) wa ndani wa jani la mmea wa mshubiri ukiwa freshi na upake sehemu yote ya ndani ya uke wako mara 2 mpaka 3 kwa siku kwa wiki 3 hadi 4 na hutakawia kuona matokeo mazuri. Matumizi ya jeli ya aloe vera kusaidia kupunguza uwezekano wa uke kulegea. Aloe Vera ni dawa asili iliyothibitika kukaza uke kwa asili bila madhara yoyote mabaya. Ina vitamini nyingi zikiwemo vitamini A, C, folic acid, choline na madini kama zinki, magnesiamu, kalsiamu na sodiamu vyote hivi ni mhimu katika kuhamasisha kukazika kwa uke kwa ujumla. Mmea huu wa asili hauna ugumu wowote katika matumizi yake. Tumia tu jeli kutoka katika jani freshi la mu-aloe vera na utumie vidole vyako kusambaza ndani ya uke. Kama jeli hii ikichanganywa na mate kabla ya kupaka ukeni inaweza kutumika kama dawa bora ya kulainisha pia uke mkavu na kufanya tendo la ndoa lenye kuvutia sana. Nina uhakika kuwa hii siyo mara yako ya kwanza kusikia kuhusu kazi hii ya mmea huu. Mshubiri unatumika katika bidhaa nyingi za vipodozi za asili.
5. Zabibubata (Gooseberry) Zabibubata ni moja ya dawa asili nzuri zaidi katika kukaza kuta za kifaa chako. Chemsha kwenye moto zabibubata 10 mpaka 12 ndani ya maji upate kama supu hivi nzito. Kisha mimina kwenye chupa safi na utunze sehemu safi na salama. Pakaa hiyo dawa kila siku ndani ya uke wako dakika 10 kabla ya kwenda kuoga. Hii itaongeza uwezo wa kujibana tena kwa misuli ya kifaa chako. Kwa hakika zabibubata ndiyo moja ya dawa asili za kubana uke wako tena ambazo unatakiwa uzijaribu huku ukiongeza matunda haya kwenye chakula chako kila mara.
6. Mtindi Njia nyingine nzuri ya kushughulika na tatizo hili ambayo nataka kukufunulia kwenye makala hii kwako wewe msomaji wangu ni matumizi ya mara kwa mara ya mtindi. Hii ni kwa sababu mtindi unao bakteria wazuri wanaohitajika ili kuuacha uke katika afya nzuri muda wote. Vile vile ukitumia mtindi kila siku ni namna nzuri ya kutibu maambukizi mbalimbali katika uke. Kikombe kimoja kwa siku (robo lita) inatosha. Unaweza pia kuweka kijiko kidogo kimoja cha chai cha mtindi ndani ya uke wako wakati unaenda kulala na uusambaze vizuri sehemu yote ya ndani ya uke wako. Mtindi unaweza kutumia wa nyumbani au hata ule wa dukani ni sawa.
7. Kitunguu swaumu Kitunguu swaumu kinaweza kuwa msaada katika kutibu baadhi ya maambukizi yaliyosababishwa na fangasi. Kutumia kitunguu swaumu mara kadhaa kwa wiki inaweza kuwa njia nyingine nzuri katika kusaidia uke wako kubaki salama na wenye afya. Vile vile kitunguu swaumu husaidia kuondoa harufu mbaya katika kifaa chako. * Chukuwa kitunguu swaumu kimoja * Kigawanyishe katika punje punje * Chukua punje 3 au 4 * Menya punje moja baada ya nyingine * Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10 * Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...
-
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike ki...
-
Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho l...
-
Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unak...
So useful thank you
ReplyDeleteGood
ReplyDelete