VISABABISHI VYA TATIZO HILI
sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili:
(1)BACTERIA VAGINOSIS .Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.
(2)TRICHOMONAS .maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili.
(3)YEAST INFECTION.kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina)
~maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa na tendo la ndoa, mambo ambayo huchangia tatizo hili ni i)MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA.
ii) MAWAZO
iii)UJAUZITO
iv)KISUKARI NA MATUMIZI YA ANTIBIOTICS
(4)VAGINAL OR CERVICAL CANCER.mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba
(5)SEXUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs)~Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili
(6)POOR HYGIENE ~tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo
DALILI ZA TATIZO HILI
~kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake
@UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU
~huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga
@UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA
~Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo
@UCHAFU MWEUPE MZITO KAMA JIBINI
~mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
@UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI
~uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE. Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo
👉EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
👉EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
👉PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
👉TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
👉SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA KUZIPIGA PASI
👉KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
👉EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
👉EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...
-
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike ki...
-
Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho l...
-
Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unak...
No comments:
Post a Comment