1.PENDELEA KUTUMIA MAZIWA YA MTINDI.Maziwa mtindi (yogurt) yana virutubisho ambavyo husaidia bakteria wanaopatikana ukeni kuwa katika hali ya usawa kwani wakizidi au kupungua kuweza kusababisha matatizo kama uwepo wa fangasi ukeni (yeast infection).Unaweza kulinda bakteria hawa ndani ya mwili wako kwa kufanya mtindi kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku. Kula mtindi ni njia nzuri ya kuzuia na kutibu maambukizi ya fangasi ukeni. Pia vilevile kuna vidonge vya kumeza aina ya yogurt pill ambavyo hutumika kama mbadala wa maziwa mtindi, vidonge hivi hupatikana kwenye maduka ya dawa baridi haswa yale makubwa.
2.PENDELEA KULA MATUNDA MENGI. Matunda mengi kama Cranberries, mananasi, husaidia kusafisha na kutoa harufu ya maji yaliyofunikwa na uke. Kula matunda mara kwa mara kutaifanya harufu yako ya uke kuwa nzuri mda wote. Matunda pia yanasaidia kuongeza maji mwilini na pia husaidia husafirisha na kutoa sumu mwilini ambayo inaweza kusababisha harufu mbaya.
3.TUMIA VITUNGUU SWAUMU. Vitunguu swaumu vina virutubisho ambavyo huua yeast wanaosababisha tatizo la fangasi ukeni, na kuifanya kuwa tiba nzuri ya kuzuia na kutibu magonjwa ya fangasi uJesu pamoja na kuondoa harufu mbaya. matumizi ya kitunguu kibichi au kilichopikwa mara kwa mara katika wiki husaidia uke wako kuwa na afya.
4.FANYA MAZOEZI YA KEGEL MARA KWA MARA. Mazoezi ya Kegel huimarisha misuli ya sakafu ya pelvic na misuli ya pubococcygeus. Misuli hii huregea na kuwa dhaifu kutokana na kuongezeka umri na baada ya kujifungua. Kuimarika kwa misuri hii kunaweza kukusaidia kuepuka tatizo la kushindwa kubana mkojo na pia husaidia kuongeza radha ya tendo la ndoa. Ili kufanya mazoezi ya kegel, fuata hatua hizi: Cha kwanza ni kuhakikisha hauna mkojo kisha kinachofata kuutafuta msuli huu wa kegel kwa kutumia hisia ambapo utafanya kama unabana mkojo, ukihisi kama kuna kitu kinachobana na kuachia tambua huo ndio msuli wa kegel. Kuimarisha msuli huu wa kegel ni kuubana na kushikilia kwa sekunde tatu, kisha unaachilia. Kurudia mara 15 hivi kwa siku. Endelea kufanya mazoezi ya kegel kila siku, ushikilia kwa muda mrefu na kuongeza mara kwa mara zaidi kwa wakati unaoweza kudhibiti wewe Mwenyewe.
No comments:
Post a Comment