Maambukizi kwenye njia ya uzazi au kwa kifupi PID, ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi.moja ya athari za PID ambayo wanawake hupata ni kutoweza kushika mimba yaani ugumba.
Tafiti zinasema kati ya wanawake nane walaiowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba kwa siku za hapo baadae huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati.
Nini kinasababisha PID?? Wataalamu wa afya wanaamini kwamba magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa ipasavyo hasahasa gonorrhea na chlamydia yanaongoza kwa kusababisha PID, japo kuna baadhi ya wanawake wanaugua PID kuna kwenye maambukizi ya kawaida ya bacteria(bacteria vagonosis)
NI NINI MAANA YA PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID).
Maana halisi ya PID ni hali ya kututumka au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke, sehemu hizi ni kama mirija ya uzazi au ovary ambako kunasababishwa na magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono.
Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix). Maambikizi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata Ectopic pregnancy ambayo ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija.
Dalili Za Pelvic Inflammatory Disease(PID)
Dalili za PID zinatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa baadhi ya wanawake dalili huwa mbaya na kwa wengine dalili huwa za kawaida, wakati mwingine wanawake hukaa na ugonjwa kwa muda mrefu bila kujua kutokana na kuchanganya dalili na magonjwa mengine.zifuatazo ni dalili zinazojotokeza zaidi kwa wanawake wengi
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto
Sehemu za uke kuwa na ulaini sana
Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupeleekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo la ngono na hivo kukosa tena hamu ya tendo la ndoa
Kuvurugika kwa hedhi
Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani
Maumivu wakati wa kukojoa
Kupata maumivu wakati wa choo
Kupata dalili za homa kama kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.
Madhara Yanayosababishwa Na Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi(PID)
Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha athari kubwa sana kwa mwanamke,kama tulivoona pale juu PID inaweza kusababisha ugumba na mimba kujishikiza mahali pasipo sahihi(ectopic pregnancy) tofauti na mfuko wa mimba. Kadiri unavoumwa zaidi PID ndivyo hatari ya kupata ugumba inavoongezeka. Mimba kutokea nje ya mfuko wa mimba ni ishu kubwa ya kiafya na inahitaji uangalizi mkubwa wa kidactari ili kuzuia kuvuja kwa damu na hatimae kupelekea kifo kwa mama.
MADHARA MENGINE YA PID NI:
1.Kupata majeraha kwenye mirija ya uzazi, majeraha yanaweza kutokea nje ama ndani, tatizo hili linaweza kuwa gumu kutibika na hutokea tu pale ambapo maambukizi hayakutibiwa kwa muda mrefu zaidi.
2.Kuziba na kujaa maji kwa mrija ya uzazi(hydrosalpinx kutokana na majeraha ya tishu zake.
3.Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba.
Kumbuka PID Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa vizuri (sexual transmitted diseases).
Kwa hivo basi ni muhimu kufahamu dalili za magonjwa ya zinaa ambayo ni common sana kwenye jamii yetu kama gonorrhea(kisonono) na chlamydia. Ugonjwa wa Chylamidia ni ugonjwa wa zinaa unaowaathiri wake kwa wanaume na husambazwa kupitia uke, njia ya haja kubwa na pia ngono ya mdomo.
Magonjwa haya ya ngono ambayo yanasababisha PID huwa na dalili karibu sawa na dalili PID. Dalili zngine ni kama
Kutokwa na uchafu kupita kiasi wenye rangi ya njano na kijanina unaonuka kwenye uke
Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa haja kubwa
Kutokwa na uchafu mweupe kwenye uume unaoambatana na maumivu makali
Maumivu na kuvimba kwa kende/mapumbu
Kwa baadhi ya watu hupata maumivu mahala pa haja kubwa na kutokwa na uchafu
Ugonjwa Wa PID .
Je Zipi Ni Tabia Hatarishi Zinazopelekea Uugue PID.
Kwa kiasi kikubwa wanawake waliopo chini ya umri wa miaka 35 wanaathirika zaidi na maambukizi kwenye njia za uzazi, kutokana na kwamba wanajihusisha zaidi na ngono. Tumeona hapo juu kwamba kutokutibiwa vyema kwa maradhi ya gonorrhea na chlamydia ndio chanzo kikubwa cha PID, achilia mbali sababu hii, baadhi ya bacteria wengine wanaweza pia kusababisha PID, bacteria wengine wanaweza kuambukizwa wakati wa tendo la ngono, au wakati wa kujifungua, au kwenye kitendo cha utoaji mimba na kisha wakajificha kwenye njia ya uzazi wakaanza kukua taratibu na kusambaa.baadhi ya bacteria ambao wamegundulia kusababisha PID ni hawa wafuatao
Chlamydia trachomatis
Neisseria gonorrheae
Mycoplasma genitalium
Mazingira Na Sababu Hatarishi Zinaongeza Uwezekano Wa Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID)
Kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35
Kufanya ngono bila kinga
Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi.
Kusafishwa kizazi mara kwa mara na matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu bacteria wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus
Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi
Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID
Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.
Hatua 5 Zifuatazo Zitakusaidia Kuzuia Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Na Magonjwa Ya Zinaa
1.Fanya ngono salama kwa kutumia kinga na kuishi na mpenzi mmoja mwaminifu.
hii ni hatua muhimu ya kwanza na ya uhakika zaidi katika kuzuia kupata PID maana tayari tumeshaona hapo juu kwenye makala yetu njia kubwa ya kusambaa kwa maambukizi ni ni njia ya ngono. Kama ukichagua kuwa na wapenzi wengi basi hakikisha unavaa condom kwa kila tendo. Kama una mpenzi mmoja na kati yenu kuna ambaye kaugua basi hakikisheni mnaacha kufanya ngono mpaka pale mtakapotibiwa mkapona kabisa.
2.Hakikisha unafanya vipimo kwa magonjwa ya zinaa na kuyatibu haraka iwezekanavyo
wataalamu wa afya wanashauri kwamba watu walioko chini ya miaka ishirini na tano wafanye vipimo kila mwaka kwa magonjwa ya zinaa kama chlamydia. Wanawake wenye wapenzi wengi wanatakiwa kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake(gynecologist) kwa vipimo kugundua uwepo wa vimelea vya magonjwa ya zinaa.ni muhimu kufanya vipimo mapema na kutibu mapema ugonjwa, kwa maneno mazuri ni kwamba kadiri unavochelewa kutibu magonjwa ya zinaa ndivyo unaongeza hatari zaidi ya kupata athari kubwa kwenye uzazi.
Jikinge na maradhi ya bacteria na maambukizi mengine:
3.Tumia sabuni zisizo na harufu kali(mild soap) kujisafisha- kuosha uke kwa kutumia sabuni zenye harufu kali na kemikali hufanya tishu za uke kututumka, kuharibu uwiano wa bacteria kenye uke na pia kupunguza tindikali iliyopo mpaka kupelekea kuongezeka kwa uchafu unaotolewa
Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.
4.Hakikisha unaimarisha kinga yako ya mwili : unapokuwa na kinga imara basi unajikinga dhidi ya kushambuliwa na magonjwa ya zinaa. Unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili upate virutubisho vya kuimarisha kinga yako.
5.Epuka kujisafisha mara kwa mara ukeni. Kujisafisha kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...
-
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike ki...
-
Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho l...
-
Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unak...
No comments:
Post a Comment