Sehemu ya sili (uke), ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima na wanaume na sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi na kutazamwa muda wote.
Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na
ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo.
Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa
kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako
kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama.
Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani kwa mara ya mwisho au ni mara ngapi kwa mwaka unakwenda hospitali kucheki afya yako ya ndani? Au kucheki afya yako ya kizazi?
Fahamu ya kwamba maradhi yoyote kuanza taratibu na ukua kadri siku zinavyokwenda Utakubaliana na mimi kwamba eneo hilo muhimu na nyeti halijathaminiwa kwa wanawake walio wengi.
Utafiti umebaini baadhi ya vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake wengi ni;
i) Vyoo vya kuchangia (public toilets)
Eneo hili ni hatari sana katika kusababisha maambukizi.kwa hiyo unahitaji kuwa
mwangalifu sana sehemu yoyote yenye mikusanyiko ya watu ambayo itawalazimu
(kuchangia vyoo kama; maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk...
ii) Kutotumia maji safi na salama.
Maji mengi tunayotumia sio safi na salama mengi yana bacterias. Wengine eti hujazia maji ndani ya ndoo halafu huwekwa chooni. Maji hayo huhifadhi bacterias ni hatari sana.
iii) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio salama.
Utafiti pia umebaini wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, wengine hupata michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri. Kwasababu tu wametumia pads ambazo sio salama.
iv) Bacterias
Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani.
Pia unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kupiga pasi kabla ya kuvaa. Swali, ni wanawake wangapi wanapiga pasi nguo zao za ndani kabla ya kuvaa?
Vyanzo ni vingi sana, suluhisho ni nini? "Kinga ni bora kuliko tiba " ni vyema ukafahamu namna ya kumdhibiti muhalifu kabla hajaingia ndani kwako kuliko kupambana nae akiwa tayari ndani ni ngumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...
-
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike ki...
-
Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho l...
-
Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unak...
No comments:
Post a Comment