1. Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La ndoa
Hii ni hali anmbayo huwapata wanawake ambapo hawatasikia hamu ya kufanya tendo la ndoa (loss of sexual drive or loss of libid o). Mara nyingi wanawake waliolalamika kuhusu tatiza hili ni wale ambao wamezaa na wanadai tatizo lilitokea mara ya baada ya uzazi. Kuna njia za kutatua tatizo hili kama tutakavyoona wakati tutakapoichambua mada hii kwa kina.
2. Kutokufika Kileleni
Kutokufika kileleni (loss of orgasm) ni tatizo MPambalo ni kubwa hasa katika nchi zetu. Usishangae kuona wakati tunajadili mada hii halafu mwanamke akauliza – “Hivi kwani kufika kileleni ni nini?.” Hili ni swali la kawaida miongoni mwa akina dada au akina mama hapa kwetu. Wenzetu wanatofautisha kufika kileleni kwa namna mbili – clitoral orgasm na vaginal orgasm. Unayajua hayo? Ni ukweli kwamba kuna wanawake wanaokuja kubahatika kufika kileleni miaka mingi (hata zaidi ya 10) baada ya ndoa zao na wengine hawajui kabisa kufika kileleni katika maisha yao yote.
3. Uyabisi Wa Sehemu Nyeti (Vaginal Dryness )
Mwanamke anapokuwa tayari kwa kufanya tendo la ndoa kuna ute unaotoka sehemu zake nyeti ili kulainisha maungo yake. Endapo ute huo hautatoka au ukitoka kwa kiwango kidogo sana, mwanamke atasikia maumivu wakati wa tendo zima. Hali hii ndio tuliyoiita “uyabisi wa sehemu nyeti.”
4. Maumivu Wakati Wa Kufanya Tendo La ndoa
Kuna wanawake wengine hupata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kutokana na sababu nyingine nyingi tofauti na uyabisi tulioutaja hapo juu. Utatuzi wa suala hili utategemea hali inayotokea au maelezo kutoka kwa mwenye tatizo hili.
5.Kutokwa na uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele.
6.Kuwa na uke uliolegea na kutanuka. Ambapo hili huwafanya wanawake wengi kukosa raha ya tendo la ndoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...
-
1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike ki...
-
Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho l...
-
Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unak...
No comments:
Post a Comment