Tuesday, January 1, 2019

KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.

VISABABISHI VYA TATIZO HILI

sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili:

(1)BACTERIA VAGINOSIS .Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.

 (2)TRICHOMONAS .maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili.

 (3)YEAST INFECTION.kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina) ~maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa na tendo la ndoa, mambo ambayo huchangia tatizo hili ni i)MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA.
ii) MAWAZO
iii)UJAUZITO
iv)KISUKARI NA MATUMIZI YA ANTIBIOTICS

 (4)VAGINAL OR CERVICAL CANCER.mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba 

(5)SEXUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs)~Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili (6)POOR HYGIENE ~tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo

 DALILI ZA TATIZO HILI ~kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake

 @UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU ~huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga

@UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA ~Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo

@UCHAFU MWEUPE MZITO KAMA JIBINI ~mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

@UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI ~uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE. Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo

 đź‘‰EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
 đź‘‰EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
👉PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
👉TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
👉SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA KUZIPIGA PASI
👉KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
👉EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
👉EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI.

MAZOEZI YA KUKAZA UKE ULIOLEGEA

Fanya mazoezi yafuatayo KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unakojoa kidogo unaacha kwa sekunde 10 tena unakojoa hivyo hivyo huku unapumzika mpaka unamalaiza. Fanya zoezi hili mara 3 mpaka 4 kwa siku ukienda kupata haja ndogo.

Zoezi hili kwa mjibu wa watafiti ni kuwa linasaidia kukaza misuli ya uke. SQUATS – Hili ni zoezi lingine zuri la kubana uke uliolegea. Ni kusimama na kuchuchumaa, kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo mara 15 kwa mizunguko mitano mara 2 kila siku.

Zoezi hili linasaidia pia kuwa na maungo mazuri na faida nyingine nzuri za kiafya. LEGS UP – Lala chali kisha nyanyua mguu mmoja juu kisha shusha chini na unyanyuwe mguu mwingine juu na ushushe chini hivyo hivyo mguu mmoja juu kisha chini, kisha mwingine juu chini ukichoka unapumzika kisha unaendelea hivyo hivyo kila siku kwa dakika 15 mpaka 20 mpaka kifaa chako kitapokuwa sawa

ZIJUWE SABABU ZA UKE KUWA MKUBWA

Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho la kuwa na uke mdogo.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuwa na uke mkubwa na kushiriki tendo la ndoa mara nyingi. Pia hakuna uhusiano wa umri na ukubwa wa uke. Wapo wamama watu wazima wana uke mdogo pia kuna wasichana wadogo kabisa wana uke mkubwa kupitiliza.

 Watu wengine huamini kuwa mwanamke mwenye uke mkubwa na mlegevu ametembea na wanaume wengi sana, jambo hilo sio kweli kwani hakuna uume unaoweza kufanya hivyo ila mwanamke aliyezoea uume mkubwa anaweza kupata shida kufurahia tendo la ndoa akipata mwanaume mwenye uume mdogo.

 Dalili na jinsi ya kutambua kama uke wako ni mkubwa:

1. Kama ukiingiza kidole chako ukeni inakuwa vigumu kukibana kwa uke wako 

2. Unapokuwa bado hujapata hamu ya kufanya mapenzi,uke wako (tundu ambalo uume huuingia) linakuwa wazi yaani hupati pingamizi lolote ukiingiza kidole.

 3. Unaweza kuingiza vidole vitatu au zaidi ndani ya uke wako bila kipingamizi kikubwa.

 4. Unapata shida kubwa kufika kileleni. 

Sababu kuu 10 za UKE kulegea na kuwa mkubwa.

 1. Kuzaa mara kwa mara
 2. Uzito na unene uliozidi
 3. Kujifungua kwa upasuaji
 4. Kuinua vitu vizito mara kwa mara
 5. Mazoezi mazito ya mara kwa mara
 6. Misukosuko ya siku za nyuma katika nyonga
 7. Ukomo wa hedhi
 8. Maumivu sugu nyuma ya mgongo
 9. Kupiga chafya au kikohozi mara kwa mara
 10. Kufunga choo au kupata choo kigumu mara kwa mara

BANA UKE WKO KWA KUTUMIA NJIA HIZI


1. Mbegu za uwatu Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike kisha acha kwa usiku mzima mpaka asubuhi. Asubuhi kunywa hayo maji na ule hizo mbegu pia. Fanya zoezi hili mara 3 TU kwa wiki na uenndelee na zoezi hili mpaka kifaa chako kimerudi na kuwa kidogo. Hii inasaidia pia kupunguza uzito. Mhimu – Wanawake wajawazito au wenye saratani ya matiti wasitumie dawa hii.

 2. Unga wa mbegu za embe Unga wa mbegu za embe ni dawa nyingine nzuri unaweza kutumia kukaza misuli ya uke wako uliolegea. Ukishakula embe chukua ile kokwa yake ya ndani na uianike juani, ikikauka chukua na uisage upate unga wake. Changanya unga huu na asali kidogo kisha pakaa ndani ya kuta na sehemu yote ya ndani ya uke kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa na uke wako utarudi na kuwa wa kawaida. Mbegu za embe ni chanzo kizuri cha wanga, mafuta, protini, vitamini E, nyuzinyuzi, magnesiamu, vitamini B12, asidi amino nyingi nk.

 3. Vitamini E Kwa mjibu wa utafiti kuhusu faida za vitamini E ni moja ya vitamini mhimu sana ambazo ni mhimu kwa ajili ya afya bora ya mwili. Inapendekezwa kama dawa ya kutibu kisukari na shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito. Hata hivyo wanawake wengi hawafahamu ukweli kwamba vitamini E ni dawa nzuri kwa uke mkavu na kufanya kuta za uke zenye afya na nguvu kama itatumika vizuri. Unahitaji upate mafuta ya vitamini E na uwe unaweka ukeni moja kwa moja mara 1 kwa siku mpaka utakapopata uponyaji unaouhitaji. Huwa kama kidonge hivi lakini ni mafuta na kinapasukia chenyewe ndani ya uke na kusambaa bila shida yoyote.

 4. Jeli ya mshubiri freshi Kutumia jeli ya mshubiri au aloe vera ni moja ya njia rahisi ya asili ya kukaza uke wako. Kutumia njia hii kwangua jeli (utomvu mweupe) wa ndani wa jani la mmea wa mshubiri ukiwa freshi na upake sehemu yote ya ndani ya uke wako mara 2 mpaka 3 kwa siku kwa wiki 3 hadi 4 na hutakawia kuona matokeo mazuri. Matumizi ya jeli ya aloe vera kusaidia kupunguza uwezekano wa uke kulegea. Aloe Vera ni dawa asili iliyothibitika kukaza uke kwa asili bila madhara yoyote mabaya. Ina vitamini nyingi zikiwemo vitamini A, C, folic acid, choline na madini kama zinki, magnesiamu, kalsiamu na sodiamu vyote hivi ni mhimu katika kuhamasisha kukazika kwa uke kwa ujumla. Mmea huu wa asili hauna ugumu wowote katika matumizi yake. Tumia tu jeli kutoka katika jani freshi la mu-aloe vera na utumie vidole vyako kusambaza ndani ya uke. Kama jeli hii ikichanganywa na mate kabla ya kupaka ukeni inaweza kutumika kama dawa bora ya kulainisha pia uke mkavu na kufanya tendo la ndoa lenye kuvutia sana. Nina uhakika kuwa hii siyo mara yako ya kwanza kusikia kuhusu kazi hii ya mmea huu. Mshubiri unatumika katika bidhaa nyingi za vipodozi za asili.

 5. Zabibubata (Gooseberry) Zabibubata ni moja ya dawa asili nzuri zaidi katika kukaza kuta za kifaa chako. Chemsha kwenye moto zabibubata 10 mpaka 12 ndani ya maji upate kama supu hivi nzito. Kisha mimina kwenye chupa safi na utunze sehemu safi na salama. Pakaa hiyo dawa kila siku ndani ya uke wako dakika 10 kabla ya kwenda kuoga. Hii itaongeza uwezo wa kujibana tena kwa misuli ya kifaa chako. Kwa hakika zabibubata ndiyo moja ya dawa asili za kubana uke wako tena ambazo unatakiwa uzijaribu huku ukiongeza matunda haya kwenye chakula chako kila mara.

 6. Mtindi Njia nyingine nzuri ya kushughulika na tatizo hili ambayo nataka kukufunulia kwenye makala hii kwako wewe msomaji wangu ni matumizi ya mara kwa mara ya mtindi. Hii ni kwa sababu mtindi unao bakteria wazuri wanaohitajika ili kuuacha uke katika afya nzuri muda wote. Vile vile ukitumia mtindi kila siku ni namna nzuri ya kutibu maambukizi mbalimbali katika uke. Kikombe kimoja kwa siku (robo lita) inatosha. Unaweza pia kuweka kijiko kidogo kimoja cha chai cha mtindi ndani ya uke wako wakati unaenda kulala na uusambaze vizuri sehemu yote ya ndani ya uke wako. Mtindi unaweza kutumia wa nyumbani au hata ule wa dukani ni sawa.

 7. Kitunguu swaumu Kitunguu swaumu kinaweza kuwa msaada katika kutibu baadhi ya maambukizi yaliyosababishwa na fangasi. Kutumia kitunguu swaumu mara kadhaa kwa wiki inaweza kuwa njia nyingine nzuri katika kusaidia uke wako kubaki salama na wenye afya. Vile vile kitunguu swaumu husaidia kuondoa harufu mbaya katika kifaa chako. * Chukuwa kitunguu swaumu kimoja * Kigawanyishe katika punje punje * Chukua punje 3 au 4 * Menya punje moja baada ya nyingine * Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10 * Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

MAGONJWA YA ZINAA

Mambukizi ya magonjwa ya zinaa hutokea pale maji maji ya mwili kama vile mate, damu, manii, majimaji ya ukeni kutoka kwa mtu ambae tayari ameambukizwa, yatatangamana na ya mtu ambae hajaambukizwa. Hii mara nyingi hufanyika wakati wa ngono ya kuingiliana kimwili, au ya kunyonyana sehemu za siri.

Baadhi ya majonjwa hayo (lakini sio yote) yanatibika, lakini yasipotibiwa yanaweza kusababisha madhara ya kudumu. Kumbuka maambukizi ya ukimwi na virusi vya HIV pia mara nyingi hufanyika kupitia kufanya ngono. Na kumbuka pia bado hakuna tiba ya Ukimwi, wala chanjo dhidi ya virusi vya HIV. Kwa sasa hivi kinga bora dhidi ya magonjwa ya zinaa, ni kutofanya ngono kabisa au kutumia kondom kwa kufuata maagizo kikamilifu, na kufanya ngono iliyosalama Nitajua vipi kama nimeambukizwa magonjwa yanayoathiri afya ya uzazi? Wanawake: Maji maji au ute unaotoka kwenye uke ni sawa kabisa, lakini wanawake wanapaswa kutafuta usaidizi wa kimatibabu wakigundua lolote kati ya yafuatayo:-

i).Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida.
ii).Maumivu au kusikia kama unachomeka au mwasho wakati wa kwenda haja ndogo.
iii).Maumivu na mwasho katika maeneo ya uke.
iv).Maumivu ya ukeni wakati wa kufanya ngono.
v). Vidonda na malengelenge katika eneo la uke.

Kumbuka, baadhi ya maambukizi huenda yasiwe na dalili. Hii haimaanishi kwamba huwezi kumwambukiza mpenzi wako, au kwamba hayawezi kukudhuru kiafya. Kama una wasi wasi, ni vyema kuchunguzwa na daktari haraka iwezekanavyo, ama katika kliniki.

 Wanaume: Mwanaume anapaswa kuenda kutafuta ushauri wa daktari kama atajipata na dalili zifuatazo: Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi. Kuhisi mwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo Vijidonda na sugu ama malengelenge juu au katika sehemu za kiume. Vipele au uvimbe katika sehemu za siri. Kwa mara nyingine tena, kumbuka maambukizo mengine kama ya virusi vya ukimwi yanaweza kuwemo mwilini kimya kimya kwa mda bila dalili zozote kujitokeza. Unaweza kuwa hutaona dalili yoyote kwanza, lakini haimaanishi kwamba huwezi kuwaambukiza wengine.

Kama umefanya mapenzi bila kutumia kinga na una wasi wasi huenda umeambukizwa, nenda ukafanyiwe uchunguzi na daktari.

Magonjwa ya kawaida yanayoambukiza sehemu za siri (viungo vya uzazi):

1. CYSTITIS Huu ni uvimbe mgumu Huambukiza kupitia bacteria ambazo huishi chini ya ngozi, eneo la sehemu za siri na hata kwenye utumbo mkubwa. Dalili: Dalili kubwa ni maumivu makali wakati wa haja ndogo, na kujisikia kutaka kwenda chooni mara kwa mara. Maumivu hayo yanaweza kuendelea kuwa makali kwa haraka sana. Huwakumba zaidi wanawake hasa wakati wa hedhi na wakati wa hali fulani nyenginezo kama vile kuwa na uja uzito, au kuugua ugonjwa wa sukari. Usipotibiwa kwa haraka unaweza kusambaa hadi kwenye figo na kusababisha madhara mabaya zaidi.

Matibabu:

Kunywa maji kwa wingi au vinywaji majimaji kama maji ya matunda (juisi hasa ile ya cranberry yafaa zaidi!) Unapoona tu dalili za kwanza kwanza, juisi hiyo inaweza kusaidia sana. Hata hivyo ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi na atakupendekezea dawa zinazokufaa.

2. THRUSH Huu ni ugonjwa wa kuvimba vimba ndani kwa ndani mwilini. Kwa kawaida husababishwa na 'fungus'- kukua kupita kiasi kwa kitu kama hamira. Ugonjwa huu unaweza kusambazwa kwa njia ya ngono lakini pia unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine, kwa mfano kama kuvaa chupi, suruali iliyokubana zaidi, au kama unaugua ugonjwa wa sukari. Ugonjwa huu unaweza kuwapata wanawake kwa wanaume.

Dalili:
Dalili kubwa kwa wanawake, ni kupata maumivu na kujikuna kwenye mashavu ya upenyo wa uke na sehemu ya kupitishia haja kubwa (mkunduni). Yaani kujihisi mfano wa kuanza vidonda katika eneo la sehemu za siri. Hali hiyo huandamana na kutokwa na majimaji mazito meupe kutoka ukeni yenye harufu kama hamira. Sehemu hizo huenda zikawa nyekundu zaidi, wanaumenao, huenda wakahisi mwasho kwenye uume, hasa nchani … (kichwa cha mboo) na kuhisi kama karaha ya kupata vidonda. Pia wakati mwingine uume hutokwa na majimaji au ute mzito wa njano . Matibabu: Pindi ukigunduliwa ugonjwa wa Thrust hutibika kwa usahisi. Daktari hupendekeza vidonge au krimu maalum ambazo zinapatikana kwa wingi, kwenye maduka ya madawa.

3.Trichomonas vaginalis – kwa kifupi (TV) Hiki nacho ni kijidudu cha bacteria, kidogo kinachoambukiza kupitia ukeni na kwenye mrija wa kupitishia mkojo.

 Dalili: Dalili za ugonjwa huu ni vigumu kuzigundua … hasa kwa wanaume. Dalili kwa mwanamke aliyeambukizwa ni kutokwa na majimji au ute wa rangi ya kijani – manjano hivi, ambao huenda ukawa na harufu kama ya samaki. Matibabu: Ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa urahisi, kwa madawa maalam ya kupambana na viini antibiotics. Ili kuepuka kuambukizwa upya, na kusambaa zaidi kwa ugonjwa huu inabidi mpenzio pia nae atibiwe. Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono Magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono ni baadhi ya maambukizi yanayotokea mara kwa mara kote ulimwenguni, na huwaathiri watu wa kila rika na asili, wanawake kwa wanaume. Bora tu wewe hufanya ngono, iwe ya baina ya mke na mume, au iwe baina ya wasenge au wasagaji, ama kushiriki katika aina iwayo ya ngono, basi ni vyema kuchukua tahadhari. Njia moja ni kutumia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi haya. Kwa mfano kutumia kondom na mpenzio, kila mara mnapofanya ngono, hadi pale nyote wawili mtakapokuwa mna hakika kabisa kwamba hakuna uwezekano wowote wa ninyi wawili kuambukizana magonjwa ya ngono. Hebu tuangalie orodha hii ya baadhi ya mengine yakuambukuzana kupitia ngono.

4. Chlamydia Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Dalili: Kwa wanawake dalili hazionekani kwa urahisi. Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes – yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha utasa. Wakati mwengine dalili hii unaweza kuiona - kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wanaume ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, kama vile uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Matibabu: Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu. Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza. Kama umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mpenzi huyo aarifiwe ili nae atibiwe pia.

5. KISONONO(Gonorrhoea) Huu husababishwa pia na bacteria. Unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono unaweza kuaathiri viungo kama vile uke, uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, na hata koo au mdomo kama ukifanya mapenzi ya kunyonyana.

 Dalili: Wanawake hutokwa na ute mwingi wa njano au kijani kutoka ukeni na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wanaume uume uliathirika hutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa. Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwambukiza wanaofanya mapenzi nao. Matibabu: Iwapo matibabu hayatapatikana kwa haraka kuna hatari ya mirija ya kupitisha mayai (fallopian tubes) kuharibika na hivyo kusababisha utasa. Kama una kisonono usifanye tena mapenzi hadi utakapofanyiwa uchunguzi na kupewa madawa ya kutibu ugonjwa. Ni muhimu sana kumfahamisha mpenzio ili nae pia atibiwe.

6. Herpes: Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni. Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri. Dalili: Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.

Matibabu: Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi. Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda. Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.

Magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo (Non Specific Urethritis kwa kifupi NSU) NSU ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bacteria yanayoathiri mfereji wa kupitisha mkojo yaani urethra. Magonjwa hayo husambazwa kwa kupitia kufanya mapenzi. Dalili: Kwa wanaume dalili kubwa ni kutokwa na ute, kutoka kwenye tundu ya uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa. Huenda ukasikia maumivu au kuwashwa-washwa. Matibabu: Majimaji yakitoka kwenye uume, isipokuwa mkojo au manii, ni lazima uchunguzwe na daktari, au nesi katika kliniki ya afya ya uzazi. Unaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge vya anti-biotics. Kaswende (Syphilis) Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi! Matibabu: Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili. Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe.

JE NI JINSI GANI NINAWEZA KUUTUNZA UKE WANGU NA KUUFANYA KUWA AFYA.

1.PENDELEA KUTUMIA MAZIWA YA MTINDI.Maziwa mtindi (yogurt) yana virutubisho ambavyo husaidia bakteria wanaopatikana ukeni kuwa katika hali ya usawa kwani wakizidi au kupungua kuweza kusababisha matatizo kama uwepo wa fangasi ukeni (yeast infection).Unaweza kulinda bakteria hawa ndani ya mwili wako kwa kufanya mtindi kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku. Kula mtindi ni njia nzuri ya kuzuia na kutibu maambukizi ya fangasi ukeni. Pia vilevile kuna vidonge vya kumeza aina ya yogurt pill ambavyo hutumika kama mbadala wa maziwa mtindi, vidonge hivi hupatikana kwenye maduka ya dawa baridi haswa yale makubwa. 

 2.PENDELEA KULA MATUNDA MENGI. Matunda mengi kama Cranberries, mananasi, husaidia kusafisha na kutoa harufu ya maji yaliyofunikwa na uke. Kula matunda mara kwa mara kutaifanya harufu yako ya uke kuwa nzuri mda wote. Matunda pia yanasaidia kuongeza maji mwilini na pia husaidia husafirisha na kutoa sumu mwilini ambayo inaweza kusababisha harufu mbaya.

 3.TUMIA VITUNGUU SWAUMU. Vitunguu swaumu vina virutubisho ambavyo huua yeast wanaosababisha tatizo la fangasi ukeni, na kuifanya kuwa tiba nzuri ya kuzuia na kutibu magonjwa ya fangasi uJesu pamoja na kuondoa harufu mbaya. matumizi ya kitunguu kibichi au kilichopikwa mara kwa mara katika wiki husaidia uke wako kuwa na afya.

 4.FANYA MAZOEZI YA KEGEL MARA KWA MARA. Mazoezi ya Kegel huimarisha misuli ya sakafu ya pelvic na misuli ya pubococcygeus. Misuli hii huregea na kuwa dhaifu kutokana na kuongezeka umri na baada ya kujifungua. Kuimarika kwa misuri hii kunaweza kukusaidia kuepuka tatizo la kushindwa kubana mkojo na pia husaidia kuongeza radha ya tendo la ndoa. Ili kufanya mazoezi ya kegel, fuata hatua hizi: Cha kwanza ni kuhakikisha hauna mkojo kisha kinachofata kuutafuta msuli huu wa kegel kwa kutumia hisia ambapo utafanya kama unabana mkojo, ukihisi kama kuna kitu kinachobana na kuachia tambua huo ndio msuli wa kegel. Kuimarisha msuli huu wa kegel ni kuubana na kushikilia kwa sekunde tatu, kisha unaachilia. Kurudia mara 15 hivi kwa siku. Endelea kufanya mazoezi ya kegel kila siku, ushikilia kwa muda mrefu na kuongeza mara kwa mara zaidi kwa wakati unaoweza kudhibiti wewe Mwenyewe.

LIFAHAMU TATIZO LA FIBROIDS

Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids? Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye uterus. Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas.

Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa. Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.

 Chanzo Cha Fibroids Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen. Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi.

Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana. Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja. Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.

 Dalili Za Fibroids Akina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba. Baadhi ya dalili za fibroids ni: – Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu – Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi – Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga) – Kupata haja ndogo mara kwa mara – Maumivu ya mgongo – Maumivu wakati wa tendo la ndoa – Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku – Maumivu ya kichwa – Maumivu kwenye miguu – Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa) – Uzazi wa shida – Mimba za shida – Kutopata mimba – Kutoka kwa mimba mara kwa mara Aina Ya Fibroids Kuna aina nne za Fibroids

 Intramural: Fibroids aina hii hukua kwenye kuta za uterus. Hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.

Subserosal fibroids: Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina. Subserosal fibroids huweza kukua na kuwa kubwa sana.

Submucosal fibroids: Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus.

Cervical fibroids: Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix). Tiba Ya Fibroids Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa. Endapo tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.

 Tiba Ya Fibroids Kwa Kutumia Dawa Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist) ambayo hutolewa kama sindano. Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka. Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate siku Zake) Pia tiba nyingine ni ya kufanya upasuaji kuondoa uvimbe.

MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA UZAZI(PID)

Maambukizi kwenye njia ya uzazi au kwa kifupi PID, ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi.moja ya athari za PID ambayo wanawake hupata ni kutoweza kushika mimba yaani ugumba.

Tafiti zinasema kati ya wanawake nane walaiowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba kwa siku za hapo baadae huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati. Nini kinasababisha PID?? Wataalamu wa afya wanaamini kwamba magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa ipasavyo hasahasa gonorrhea na chlamydia yanaongoza kwa kusababisha PID, japo kuna baadhi ya wanawake wanaugua PID kuna kwenye maambukizi ya kawaida ya bacteria(bacteria vagonosis)

NI NINI MAANA YA PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID).
Maana halisi ya PID ni hali ya kututumka au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke, sehemu hizi ni kama mirija ya uzazi au ovary ambako kunasababishwa na magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono. Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix). Maambikizi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata Ectopic pregnancy ambayo ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija.

Dalili Za Pelvic Inflammatory Disease(PID) Dalili za PID zinatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa baadhi ya wanawake dalili huwa mbaya na kwa wengine dalili huwa za kawaida, wakati mwingine wanawake hukaa na ugonjwa kwa muda mrefu bila kujua kutokana na kuchanganya dalili na magonjwa mengine.zifuatazo ni dalili zinazojotokeza zaidi kwa wanawake wengi Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto Sehemu za uke kuwa na ulaini sana Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupeleekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo la ngono na hivo kukosa tena hamu ya tendo la ndoa Kuvurugika kwa hedhi Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani Maumivu wakati wa kukojoa Kupata maumivu wakati wa choo Kupata dalili za homa kama kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi. Madhara Yanayosababishwa Na Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi(PID) Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha athari kubwa sana kwa mwanamke,kama tulivoona pale juu PID inaweza kusababisha ugumba na mimba kujishikiza mahali pasipo sahihi(ectopic pregnancy) tofauti na mfuko wa mimba. Kadiri unavoumwa zaidi PID ndivyo hatari ya kupata ugumba inavoongezeka. Mimba kutokea nje ya mfuko wa mimba ni ishu kubwa ya kiafya na inahitaji uangalizi mkubwa wa kidactari ili kuzuia kuvuja kwa damu na hatimae kupelekea kifo kwa mama.

 MADHARA MENGINE YA PID NI:
 1.Kupata majeraha kwenye mirija ya uzazi, majeraha yanaweza kutokea nje ama ndani, tatizo hili linaweza kuwa gumu kutibika na hutokea tu pale ambapo maambukizi hayakutibiwa kwa muda mrefu zaidi.

 2.Kuziba na kujaa maji kwa mrija ya uzazi(hydrosalpinx kutokana na majeraha ya tishu zake. 3.Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba. Kumbuka PID Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa vizuri (sexual transmitted diseases).

Kwa hivo basi ni muhimu kufahamu dalili za magonjwa ya zinaa ambayo ni common sana kwenye jamii yetu kama gonorrhea(kisonono) na chlamydia. Ugonjwa wa Chylamidia ni ugonjwa wa zinaa unaowaathiri wake kwa wanaume na husambazwa kupitia uke, njia ya haja kubwa na pia ngono ya mdomo. Magonjwa haya ya ngono ambayo yanasababisha PID huwa na dalili karibu sawa na dalili PID. Dalili zngine ni kama Kutokwa na uchafu kupita kiasi wenye rangi ya njano na kijanina unaonuka kwenye uke Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa haja kubwa Kutokwa na uchafu mweupe kwenye uume unaoambatana na maumivu makali Maumivu na kuvimba kwa kende/mapumbu Kwa baadhi ya watu hupata maumivu mahala pa haja kubwa na kutokwa na uchafu Ugonjwa Wa PID .

Je Zipi Ni Tabia Hatarishi Zinazopelekea Uugue PID. Kwa kiasi kikubwa wanawake waliopo chini ya umri wa miaka 35 wanaathirika zaidi na maambukizi kwenye njia za uzazi, kutokana na kwamba wanajihusisha zaidi na ngono. Tumeona hapo juu kwamba kutokutibiwa vyema kwa maradhi ya gonorrhea na chlamydia ndio chanzo kikubwa cha PID, achilia mbali sababu hii, baadhi ya bacteria wengine wanaweza pia kusababisha PID, bacteria wengine wanaweza kuambukizwa wakati wa tendo la ngono, au wakati wa kujifungua, au kwenye kitendo cha utoaji mimba na kisha wakajificha kwenye njia ya uzazi wakaanza kukua taratibu na kusambaa.baadhi ya bacteria ambao wamegundulia kusababisha PID ni hawa wafuatao Chlamydia trachomatis Neisseria gonorrheae Mycoplasma genitalium Mazingira Na Sababu Hatarishi Zinaongeza Uwezekano Wa Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35 Kufanya ngono bila kinga Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi. Kusafishwa kizazi mara kwa mara na matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu bacteria wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.

 Hatua 5 Zifuatazo Zitakusaidia Kuzuia Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Na Magonjwa Ya Zinaa

 1.Fanya ngono salama kwa kutumia kinga na kuishi na mpenzi mmoja mwaminifu. hii ni hatua muhimu ya kwanza na ya uhakika zaidi katika kuzuia kupata PID maana tayari tumeshaona hapo juu kwenye makala yetu njia kubwa ya kusambaa kwa maambukizi ni ni njia ya ngono. Kama ukichagua kuwa na wapenzi wengi basi hakikisha unavaa condom kwa kila tendo. Kama una mpenzi mmoja na kati yenu kuna ambaye kaugua basi hakikisheni mnaacha kufanya ngono mpaka pale mtakapotibiwa mkapona kabisa.

 2.Hakikisha unafanya vipimo kwa magonjwa ya zinaa na kuyatibu haraka iwezekanavyo wataalamu wa afya wanashauri kwamba watu walioko chini ya miaka ishirini na tano wafanye vipimo kila mwaka kwa magonjwa ya zinaa kama chlamydia. Wanawake wenye wapenzi wengi wanatakiwa kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake(gynecologist) kwa vipimo kugundua uwepo wa vimelea vya magonjwa ya zinaa.ni muhimu kufanya vipimo mapema na kutibu mapema ugonjwa, kwa maneno mazuri ni kwamba kadiri unavochelewa kutibu magonjwa ya zinaa ndivyo unaongeza hatari zaidi ya kupata athari kubwa kwenye uzazi. Jikinge na maradhi ya bacteria na maambukizi mengine:

 3.Tumia sabuni zisizo na harufu kali(mild soap) kujisafisha- kuosha uke kwa kutumia sabuni zenye harufu kali na kemikali hufanya tishu za uke kututumka, kuharibu uwiano wa bacteria kenye uke na pia kupunguza tindikali iliyopo mpaka kupelekea kuongezeka kwa uchafu unaotolewa Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.

 4.Hakikisha unaimarisha kinga yako ya mwili : unapokuwa na kinga imara basi unajikinga dhidi ya kushambuliwa na magonjwa ya zinaa. Unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili upate virutubisho vya kuimarisha kinga yako.

 5.Epuka kujisafisha mara kwa mara ukeni. Kujisafisha kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke.

LIFAHAMU TATIZO LA KUVIMBA UKENI

(vulvovaginitis) HIli ni tatizo kubwa ambalo huwatokea wanawake wengi ambapo hupelekea kuwashwa na kuvimba kwa sehemu za sili, kutokwa na usaha na hatimaye kusababisha uke kulegea. Kwa ujumla, dalili ya kififia uke ni kama ifuatavyo:

 1.Kuwashwa wa eneo la sili. Hili huendana sambamba na kuvimba kwa mashavu makubwa ya uke yanayoonekana kwa nje, Wakati huo huo mashavu madogo ya uke ya ndani huvuja usaha.

 2.uke kutoa harufu Mbaya. 3.Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa pamoja wakati wa kufanya mapenzi. Maambukizi ya vaginitis yanachukua asilimia 90% kati ya matatizo yote wakati wa umri wa kuzaa wa wamawanamke na inawakilishwa katika makundi matatu: Candidiasis: vaginitis unaosababishwa na albicans Candida (fangasi). Bakteria vaginosis: vaginitis unaosababishwa na Gardnerella (a bacterium Trichomoniasis: vaginitis unaosababishwa na Trichomonas vaginalis (a protozoan vimelea). Pia vile vile kikawaida maambukizi mengine yanayosababisha tatizo hili ni pamoja na ugonjwa wa kisonono, Klamidia, mycoplasma, malengelenge, campylobacter, usafi mbaya, na vimelea vya na baadhi ya wadudu tegemezi. Kwa hio ni vyema kwenda kufanyiwa utafiti ili utambulike una maumivu ya aina gani.

 JE, TATIZO HILI HUSABABISHWA NA NINI Maranyingi tatizohili husababishwa na mambo mbalimbali kama:
1.Bacteria
2.Fangasi
3.Utumiaji wa madawa ya uzazi wa mpango

Yafahamu Matatizo ya Kiafya ya Uzazi kwa Mwanamke

1. Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La ndoa Hii ni hali anmbayo huwapata wanawake ambapo hawatasikia hamu ya kufanya tendo la ndoa (loss of sexual drive or loss of libid o). Mara nyingi wanawake waliolalamika kuhusu tatiza hili ni wale ambao wamezaa na wanadai tatizo lilitokea mara ya baada ya uzazi. Kuna njia za kutatua tatizo hili kama tutakavyoona wakati tutakapoichambua mada hii kwa kina.

 2. Kutokufika Kileleni Kutokufika kileleni (loss of orgasm) ni tatizo MPambalo ni kubwa hasa katika nchi zetu. Usishangae kuona wakati tunajadili mada hii halafu mwanamke akauliza – “Hivi kwani kufika kileleni ni nini?.” Hili ni swali la kawaida miongoni mwa akina dada au akina mama hapa kwetu. Wenzetu wanatofautisha kufika kileleni kwa namna mbili – clitoral orgasm na vaginal orgasm. Unayajua hayo? Ni ukweli kwamba kuna wanawake wanaokuja kubahatika kufika kileleni miaka mingi (hata zaidi ya 10) baada ya ndoa zao na wengine hawajui kabisa kufika kileleni katika maisha yao yote.

 3. Uyabisi Wa Sehemu Nyeti (Vaginal Dryness ) Mwanamke anapokuwa tayari kwa kufanya tendo la ndoa kuna ute unaotoka sehemu zake nyeti ili kulainisha maungo yake. Endapo ute huo hautatoka au ukitoka kwa kiwango kidogo sana, mwanamke atasikia maumivu wakati wa tendo zima. Hali hii ndio tuliyoiita “uyabisi wa sehemu nyeti.”

 4. Maumivu Wakati Wa Kufanya Tendo La ndoa Kuna wanawake wengine hupata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kutokana na sababu nyingine nyingi tofauti na uyabisi tulioutaja hapo juu. Utatuzi wa suala hili utategemea hali inayotokea au maelezo kutoka kwa mwenye tatizo hili.

 5.Kutokwa na uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele.

 6.Kuwa na uke uliolegea na kutanuka. Ambapo hili huwafanya wanawake wengi kukosa raha ya tendo la ndoa.

USAFI WA SEHEMU ZA SILI

Sehemu ya sili (uke), ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima na wanaume na sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi na kutazamwa muda wote. Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo.

Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama. Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani kwa mara ya mwisho au ni mara ngapi kwa mwaka unakwenda hospitali kucheki afya yako ya ndani? Au kucheki afya yako ya kizazi? Fahamu ya kwamba maradhi yoyote kuanza taratibu na ukua kadri siku zinavyokwenda Utakubaliana na mimi kwamba eneo hilo muhimu na nyeti halijathaminiwa kwa wanawake walio wengi.

Utafiti umebaini baadhi ya vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake wengi ni;
 i) Vyoo vya kuchangia (public toilets) Eneo hili ni hatari sana katika kusababisha maambukizi.kwa hiyo unahitaji kuwa mwangalifu sana sehemu yoyote yenye mikusanyiko ya watu ambayo itawalazimu (kuchangia vyoo kama; maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk...

ii) Kutotumia maji safi na salama. Maji mengi tunayotumia sio safi na salama mengi yana bacterias. Wengine eti hujazia maji ndani ya ndoo halafu huwekwa chooni. Maji hayo huhifadhi bacterias ni hatari sana.

iii) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio salama. Utafiti pia umebaini wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, wengine hupata michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri. Kwasababu tu wametumia pads ambazo sio salama.

iv) Bacterias Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani. Pia unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kupiga pasi kabla ya kuvaa. Swali, ni wanawake wangapi wanapiga pasi nguo zao za ndani kabla ya kuvaa? Vyanzo ni vingi sana, suluhisho ni nini? "Kinga ni bora kuliko tiba " ni vyema ukafahamu namna ya kumdhibiti muhalifu kabla hajaingia ndani kwako kuliko kupambana nae akiwa tayari ndani ni ngumu.

KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI.

VISABABISHI VYA TATIZO HILI sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili: (1)BACTERIA VA...